Biashara na serikali zinahitaji haraka kuwekeza katika familia ili kupunguza umaskini na kuweka misingi wa afya ya watoto na mafanikio ya watu wazima, limesema shirika la kuhudumia watoto, UNICEF kwenye sera mpya inayoelezea ushahidi wa hivi punde zaidi na mapendekezo mapya kuhusu sera bora kwa ajili ya familia.