Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada kwa familia zenye watoto wadogo unahitajika dunia nzima: UNICEF

 wanawake katika zahanati moja kwenye kijiji cha Hassian, kaskazini  mashariki mwa Côte d'Ivoire wakisubiri watoto wao kupewa chanjo dhidi ya TB.
UNICEF/Frank Dejongh
wanawake katika zahanati moja kwenye kijiji cha Hassian, kaskazini mashariki mwa Côte d'Ivoire wakisubiri watoto wao kupewa chanjo dhidi ya TB.

Msaada kwa familia zenye watoto wadogo unahitajika dunia nzima: UNICEF

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Biashara na serikali zinahitaji haraka kuwekeza katika familia ili kupunguza umaskini na kuweka misingi wa afya ya watoto na mafanikio ya watu wazima, limesema shirika la kuhudumia watoto, UNICEF kwenye sera mpya inayoelezea ushahidi wa hivi punde zaidi na mapendekezo mapya kuhusu sera bora kwa ajili ya familia.

Sera bora kwa familia: Mabadadiliko kwenye maeneo ya kufanyia kazi yanahitaji sera kama vile likizo zinazolipwa kwa mzazi, manufaa ya kifedha, muda wa kunyonyesha, afya nafuu na iliyo bora bado havipo kwa wazazi wengi duniani.

Hakuna wakati ulio muhimu zaidi kwa maisha ya mtoto kama miaka yao ya kwanza utotoni, alisema mkurugenzi mtendaji wa UNICEF Henriarta Fore.

Alisema kuwa ndiyo sababu tunahitaji mabadiliko kuhusu ni vipi biashara na serikali zinawekeza kwenye sera ambazo haziinuia tu ukuaji wenye afya bali pia kujenga uhusiano mzuri kati ya wazazi na watoto wao kwa manufaa ya kichumi na kijamii.

Likizo za kulea zilizo na malipo

Takriban miezi sita inayolipwa kwa wazazi wote, kati ya hiyo wiki 18 zinazolipwa zitengewe mama. Serikali na biashara zinastahili kujikakamua hadi meizi 12 kwa pamoja ya likizo inayolipwa.

Karibu theluthi mbili ya wanaume na wanawake duniabu hufanya kazi za vibarua hali inayoathiri haki za kupata likizo ya kulea.

Kwenye nchi za kipato cha chini na wastani, kuongezwa kwa mwezi mmoja kwenye likizo ya kulea imegunduliwa kupungzua vifo vya watoto kwa asilimia 13.

Kwenye nchi za kipato cha juu, wiki moja zaidi kwenye likizo ya kulea inayolipwa ina uhusiano na kupungua kwa asilimia 4 ya wazazi wasio na mabwana kuishi kwenye umaskini.

Msaada kwa wanaonyonyesha: Kupata muda wakati wa kazi ili kunyonyesha na kukamua maziwa, mazingira mazuri ya kunyonyesha na uwepo kwa vifaa bora, huwawezesha akina mama kundelea kunyonyesa watoto hata baada ya kurudi kazini.

 

Takwimu za hivi punde zilionyesha kuwa ni asilimia 40 tu ya watoto walio chini ya miezi sita wanaonyonyesha kwa njia inayostahili. Maeneo ya kazi huwa kizuizi kikubwa cha unyonyeshaji huku asilimia 16 ya maeneo ya kufanyia kazi kuwa hayatoi msaada kwa suala hilo.

Unyonyeshaji huchangia kuwapunguzia magonjwa watoto na kwa matokeo mema kielimu.

Matunzo ya watoto

Matunzo mema na nafuu kwa watoto kuanzia kumalizika kwa likizo ya mzazi hadi mtoto aanze masomo.

Watoto wanaopata matunzo mema ya mapema huwa na afya nzuri, hujifunza vizuri na hukaaa shuleni kwa kipindi kirefu na pia hupata mafanikio ya juu wakiwa watu wazima.

Manufaa ya watoto

Kuongezwa kwa manufaa ya kifedha kwa watoto wote, kuanzia wale wadogo zaidi na hadi kufikia huduma zote. Manufaa kwa watoto inastahili kuwa mfumo wa kila nchi kwa watoto wadogo.

Takwimu za hivi majuzi zilionyesha kuwa familia moja kati ya tatu duniani hupokea manufaa yatokanayo na malipo ya watoto ya yakitofautiana kwa asilimia 88 huko Ulaya na Asia ya Kati, asilimia 28 huko Asia na Pacific na asilimia 16 barani Afrika, ikimaanisha kuwa asilimia kubwa ya watoto kwenye nchi maskini, wanaoishi katika familia maskini hawapati manufaa ya kifedha kusaidia ukuaji wao.