Usajili wa warejeshaji wa mazingira Afrika Kusini waleta nuru katika kazi yao ya kuchambua taka
Sisi si wakusanya taka bali ni warejeshaji wa mazingira kwa kuepusha lundo la vitu vinavyoweza kurejelezwa kutupwa kiholela kwenye madampo. Ni kauli ya Noluthando Tutani, kutoka Chama cha Warejeshaji wa Mazingira nchini Afrika Kusini (ARO) alipozungumza kupitia video ya Benki ya Dunia kuhusu mchango wao katika kulinda mazingira.