Israel inawajibika kwa vitendo vinne vya mauaji ya kimbari Gaza: Navi Pillay
Mwenyekiti wa tume huru inayochunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu katika ardhi ya Palestina Iliyokaliwa kwa mabavu na Israel leo ameiambia kamati ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba Israel imehusika na vitendo vinne vya mauaji ya kimbari huko Gaza, huku viongozi wake wakihamasisha utekelezaji wa mauaji hayo.”