Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OHCHR na AU watoa mwongozo wa kuwalinda wanawake Afrika wakati wa COVID-19

Wanawake wakiwa kwenye kituo cha afya nchini Ethiopia
World Bank/Binyam Teshome
Wanawake wakiwa kwenye kituo cha afya nchini Ethiopia

OHCHR na AU watoa mwongozo wa kuwalinda wanawake Afrika wakati wa COVID-19

Wanawake

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) na Muungano wa Afrika AU, kwa Pamoja wameandaa muongozo mpya wa uwezekano wa hatua za kuchukuliwa na mataifa ya Afrika kwa kuzingatia wajibu wao wa haki za binadamu, ili kuepuka ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana katika mapambano yao dhidi ya janga la corona au COVID-19

Ofisi hizo zimesema kama ilivyokuwa katika milipuko ya siku za nyuma ikiwemo Ebola na Zika , sera na juhudi za afya ya umma kote duniani zinaonekana hazijazingatia athari za muda mfupi na za mufa mrefu za COVID-19 katika suala la kijinsia ikiwemo haki za binadamu kwa watu walioathirika.

Yameongeza kuwa “ukweli ni kwamba hatua zilizochukuliwa zinahatarisha kuendeleza na kupanua wigo wa pengo la usawa wa kijinsia lililokuwepo na ubaguzi. Kama ilivyo sehemu zingine duniani wanawake na wasichana barani Afrika wanauwezekano mkubwa wa kubeba gharama ya athari za virusi hivyo.”

OHCHR yashirikiana na AU kuwalinda wanawake

 Hivi sasa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Afrika Mashariki inashirikiana kwa karibu na Tume ya Muungano wa Afrika ikiwemo idara ya mkurugenzi wa jinsia na kwa kuzingatia COVID-19 pande zote mbili zimeona ni muhimu kulijukulia jambo hili kutokana na uzoefu wa wanawake wa afrika na kujikita katika masuala maalum na makundi ya wanawake barani Afrika.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa ofisi ya haki za binadamu wa kikanda Nwanne Vwede-Obahor “Wajibu wa kutomwacha yeyote nyuma upo sio tu katika viwango vya kimataifa vya haki za binadamu bali pia katika viwango vya Afrika vya haki za binadamu.”

Muongozo huo uliopewa jina “Hatua saba zinazowezekana:Haki za wanawake na COVID-19” umeanzishwa ili kuzisaidia wizara za serikali barani Afrika zinazohusika na mipango na hatua za kukabiliana na COVID-19 , mashirika ya asasi za kiraia  na watetezi wa haki za wanawake wanaofanya kazi ya uchagigaziji na serikali.

“Ni nyenzo ambayo serikali na mashirika ya asasi za kiraia yanaweza kuitumia kufuatilia endapo serikali inatimiza wajibu wake na majukumu yak echini ya sharia za kimataifa za haki za binadamu” amesema Adwoa Kufuor-Owusu, mshauri wa kikanda wa masuala ya kijinsia kwenye ofisi ya haki za binadamu ya Afrika Mashariki.

Muongozo mpya wa kuwalinda wanawake

 Katika kila fungu la hatua zinazochukuliwa kukabiliana na janga la COVID-19 mwongozo huo unaainisha uwezekano wa hatua za kuchukua na hatua hizi zinapaswa kwenda sanjari na viwango vya haki za binadamu.

Kwa mfano mwongozo huo unataja kwamba asilimia 74 ya wanawake barani Afrika ndio nguvukazi ya uchumi wa sekta isiyorasmi na Ushahidi unadhihirisha kwamba athari za kiuchumi za COVID-19 zimewakumba zaidi wanawake hawa.

Mkatba wa Maputo wa katiba ya Afrika kuhusu wat una haki za binadamu na haki za wanawake Afrika unatambua kwamba kukiukwa au kutowapa haki za wanawake za kiuchumi, kijamii na kitamaduni mara nyingi huwaacha wwanawake wasiojiweza katika hatari ya ukatili zaidi.

Wanawake viongozi washerehekea baada ya kufungwa kwa warsha ya uwiano na kutatua mizozo JUba nchini Sudan Kuisni.
UNMISS
Wanawake viongozi washerehekea baada ya kufungwa kwa warsha ya uwiano na kutatua mizozo JUba nchini Sudan Kuisni.

 

Nini kifanyike

Mwongozo huo unasema ili kupunguza athari za muda mrefu kwa wanawake katika uwezeshaji wa kiuchumina kijamii na kuongeza hali ya wanawake kuwa niapanda Zaidi, serikali zinashauriwa kujumuisha sekta isiyo rasmi katika sera na hatua zenye lengo la kupunguza athari za kiuchumi zitoknazo na janga la COVID-19, kuanzisha hatua za ulipaji fidia na uwezeshaji wa kiuchumi wa wanawake ikiwemo msaada wa kifedha na ufikishaji wa huduma za msingi, na kupanua wigo wa hatua za uhakika wa ajira kwa ajili ya sekta zisizo na faida kubwa.

Pia muongozo umesema hali halisi ya wanawake wengi inawaweka katika hatari kubwa ya kupata maambukizi. Kimataifa wanawake ni asilimia 70 ya wafanyakazi katika sekta za afya na ustawi wa jamii , ni wahudumu wa kwanza na wanaosaidia wagonjwakatika familia zao.

Ajenda ya Afrika yam waka 2063 ya Muungano wa Afrika na mkakati wake kwa ajili ya ujumuishi na maendeleo endelevu inatoa wito kwa nchi zote kuchagiza afya na ustawi kwa raia wake ikiwemo kupanua wigo wa huduma bora za afya hususan kwa wanawake na wasichana.

Mwongozo pia umezishautri nchi kuchagiza usawa wa kijinsia na na mtazamo wa haki za wanawake katika mifumo yao ya afya na ndani ya mipango ya udhibiti wa COVID-19 ili kuhakikisha fursa ya huduma za afya kwa wote ikiwemo huduma ya afya ya uzazi na kuwapa ulinzi kamili wanawake watoa huduma walio katika hsekta ya afya.

Mwongozo pia unazishauri nchi kuhusu ukatili wa kijinsia, fursa ya kupata chakula, maji na usafi, ushiriki katika maamuzi, mazingira ya kibinadamu na kukusanya takwimu na taarifa.

Katika kuchukua hatua zote hizi ni muhimu kuhakikisha kwamba hatua zote zinazochukuliwa kupambana na COVID-19, zinakidhi mahitaji ya wanawake wote wakiwemo wahamiaji, wa vijijini na wenye ulemavu,” amesema Kufuor-Owusu.