Coronavirusi

30 APRILI 2020

Hii leo katika Jarida la Habari kutoka Umoja wa Mataifa Flora Nducha anakuletea

-Miezi mitatu baada ya WHO kutangaza COVID-19 kuwa janga la kimataifa Shirika hilo linasema halitokata tamaa katika juhudi za kutokomeza janga hilo.

-Kambi ya wakimbizi nchini Kenya wahudumu wa afya wanafanya kila wawezalo kuwalinda wakimbizi dhidi ya COVID-19.

-Nchini DRC kutana na mtoto Cornell anayeelimisha jamii kujikinga na janga la COVID-19 huku akiwasaidia wazazi wake.

-Makala yetu leo inatupeleka Uganda kumulika uhakika wa chakula wakati huu wa janga la COVID-19 .

Sauti
11'18"
Wanafunzi kutoka shule ya msingi ya Minyinyi, nchini Tanzania na mwalimu wao ambaye anawafundisha kutumia kifaa cha kupima rutuba kwenye ardhi kwa ajili ya vipimo vya mbolea.
FAO Tanzania

Wanafunzi Tanzania kujifunza kupitia redio na televisheni kutokana na COVID-19

Nchini Tanzania, wito wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, wa kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kujifunza hata wakati wa huu wa kusalia majumbani kutokana na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19, umeanza kutekelezwa ambapo hii leo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imezindua rasmi urushaji wa vipindi vya masomo kupitia televisheni na Radio.

Sauti
2'40"
UN Kenya/Newton Kanhema

Kenya yatangaza visa vipya vya COVID-19 na kufikisha idadi ya wagonjwa hadi 81

Wagojwa wawili ambao wamethibitishwa kupona virusi vya corona nchini Kenya wameonekaa hadharani kwa mara ya kwanza leo wakati wakizungumza kwa njia ya video na Rais Uhuru Kenyatta na kuonyeshwa kwenye runinga kadhaa nchini Kenya. Hata hivyo wizara ya afya nchini Kenya imatangaza uwepo kwa wagonjwa 22 zaidi wa virusi vya corana hii leo na kufanya idadi jumla kufikia wagonjwa 81. Jason Nyakundi anayo taarifa kamili

(TAARIFA YA JASON NYAKUNDI)

Sauti
3'31"

26 MACHI 2020

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania vyachukua hatua kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona COVID-19 ikiwemo kupunguza mrundikano magerezani

- Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema  COVID-19 isiwe chanzo cha kusahau huduma muhimu za chanjo kwa watoto

-Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limewachagiza wahamiaji kuingia katika sekta ya kilimo likisema jembe halimtupi mkulima

Sauti
12'55"