Kuanzia Libya, Yemen, Syria zahma imeighubika dunia: Guterres

4 Februari 2020

Ni lazima tuvinje mzunguko wa machafuko na zahma zinazoighubika dunia hivi sasa , “leo hii upepo mbaya imevamia dunia” amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo akizungumza na waandishi wa Habari mjini New York Marekani.

Katika mkutano huo kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa Guterres amesema “Kuanzia Libya hadi Yemen, kupitia Syria na kwengineko madhila ya kupanda mlima yamerejea, silaha zinamiminika na mashambulizi yanaongezeka”

Amesema ingawa kila hali ni tofauti lakini kilicho bayana ni kwamba kuna ongezeko la kutokuwepo na utulivu na mivutano “ambayo inafanya kila kitu kutotabirika na kutodhibitiwa na kuongeza hatari ya kufanya maamuzi mabaya”

Amesisitiza kwamba wakati huohuo maazimio ya Baraza la Usalama yanaheshimiwi wala kutekelezwa na kuonya mwaka na matatizo yanazidi kurundikana moja bada ya linguine.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amekumbusha kwamba umasikini unazidi kuwa mzigo mzito wakati uchumi unadhoofika.

"Wakati hali ya usoni inaonekana kuwa mbaya, simulizi za wapagani na kikabila zinaendelea kupendeza machoni pa wengi. Wakati kukosekana kwa utulivu kunaoongezeka, uwekezaji hukauka na maendeleo yanapungua, "amesema Guterres.

Ameonya kwamba “wakati mzozo wa silaha ukiendelea, jamii zinafikia sehemu hatari ya uvumilivu. Na kadri utawala unavyodhoofika, magaidi wanazidi kuwa na nguvu, na kuziba pengo hilo, "

Katibu Mkuu amesema atafanya kila awezalo katika mwaka ujao "kuvunja mzunguko mbaya wa mateso na migogoro na kuleta wimbi la diplomasia ya amani.”

Pia amewajulisha waandishi hao wa Habari waliokusanyika kwamba atahudhuria mkutano wa Muungano wa afrika (AU) utakaofanyika mwishoni mwa wiki mjini Addis Ababa, Ethiopia.

"Muungano wa Afrika ni moja wapo ya washirika wakuu wa mkakati wa Umoja wa Mataifa, na ninatarajia kujadili juhudi za bara la Afrika 'kunyamazisha silaha na pia kazi yetu ya pamoja kushughulikia changamoto kubwa za ulimwengu"

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza uharaka wa kushughulikia mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi na haja ya kuvunja mzunguko mbaya wa umaskini na kuziba pengo la usawa na kujenga utandawazi mzuri ambao hautomuacha mtu yeyote nyuma.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter