libya

Vifo vingi vinavyotokea bahari ya Mediteraia vinaweza kuepukika: UN

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ametoa wito kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini Libya na Muungano wa Ulaya, EU, pamoja na nchi wanachama wa Umoja huo kurekebisha haraka mfumo, sera na kanuni za sasa za kusaka na kuokoa watu kwenye bahari ya Meditera

Sauti -

Muungano wa Ulaya na Libya zatakiwa kurekebisha sera za uokoaji Mediteranea

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ametoa wito kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini Libya na Muungano wa Ulaya, EU  Pamoja na nchi wanachama wa Umoja huo kurekebisha haraka mfumo, sera na kanuni za sasa za  kusaka na kuokoa watu kwenye bahari ya Mediteranea kwa kuwa mifumo ya sasa inapora haki za uhai na utu za wahamiaji.

Asante Rwanda kwa kukubali kunusuru wasaka hifadhi walio hatarini Libya- Grandi 

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi ambaye bado yuko ziarani kwenye ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika, amezishukuru Rwanda na Niger kwa kuwezesha utekelezaji wa mpango wa kuhamisha wasaka hifadhi wanaokumbwa na madhila nchini Libya. 

Watu 130 wafa maji Libya baada ya boti kuzama:IOM 

Boti iliyozama Pwani ya Libya imeripotiwa kukatili maisha ya watu 130, licha ya kuomba msaada wa dharura wa uokozi limesema shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM. 

UNHCR mkombozi wa wakimbizi wajawazito wa Eritrea walioko Libya.

Kama sehemu ya huduma mbali mbali za ulinzi zinazotolewa kwa wakimbizi na wanaotafuta hifadhi nchini Libya, shirika la kuhudumia wakimbizi

Sauti -
2'13"

Huduma kwa wajawazito Libya zinazowezeshwa na UNHCR mkombozi wa wakimbizi wa Eritrea

Kama sehemu ya huduma mbali mbali za ulinzi zinazotolewa kwa wakimbizi na wanaotafuta hifadhi nchini Libya, shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR kupitia mdau wake, Kamati ya kimataifa ya uokozi, IRC, wanatoa huduma za afya ya uzazi bila malipo kwa wanawake ambao ni wajawazito au wamejifungua hivi karibuni, na pia kuwapatia rufaa za kwenda kwenye vituo vikubwa zaidi kwa ajili ya kujifungua.

Ndoto ya mtoto mkimbizi kuwa daktari yawezeshwa na UNICEF.

Nchini Niger watoto wakimbizi waliolazimika kukimbia Libya kutokana na ghasia za ugenini hivi sasa wanaona nuru ya maisha yao baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi

Sauti -
2'

UNICEF yawezesha mtoto mkimbizi kuwa na ndoto ya kuwa daktari 

Nchini Niger watoto wakimbizi waliolazimika kukimbia Libya kutokana na ghasia za ugenini hivi sasa wanaona nuru ya maisha yao baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNICEF, kuwapatia maeneo salama siyo tu ya kucheza bali pia kujifunza. 

Leo tuna habari njema sana katika kutafuta amani Libya-Guterres 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amekaribisha uteuzi uliofanywa na Wajumbe wa Jukwaa la Siasa la Libya na kupata viongozi wakuu wa muda kutoka pande kinzani.   

Chondechonde tuwanusuru wakimbizi na wahamiaji wanaolazimika kuvuka Mediterrania:UNHCR 

Wakati zahma zikiongezeka Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara na kuwalazimisha mamilioni ya watu kufungasha virago, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetoa raia ya kuongeza juhudi za kuwasaidia wakimbizi na wahamiaji hasa wanaobidi kupitia njia hatari kwenye bahari ya Mediterrania kwenda kusaka mustakbali bora.