Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa dunia waahidi dola bilioni 2.6  kwa ajili ya kutokomeza polio:WHO

Mama na mwana wapewa chanjo. Chanjo nyingi hutokea baada ya milipuko ya magonjwa  kama vile Polio, Kipindupindu na magonjwa mengine.
UNICEF/ Nangyo
Mama na mwana wapewa chanjo. Chanjo nyingi hutokea baada ya milipuko ya magonjwa kama vile Polio, Kipindupindu na magonjwa mengine.

Viongozi wa dunia waahidi dola bilioni 2.6  kwa ajili ya kutokomeza polio:WHO

Afya

Viongozi wa dunia, nchi na wadau mbalimbali wa afya leo wameahidi dola bilioni 2.6 zitakazotumia kutoa chanjo dhidi ya polio kwa watoto milioni 450 kila mwaka na kukabili vikwazo vya kumfikia kila mtoto na chanjo hiyo limesema shirika la afya duniani WHO.

Ahadi hiyo imetolewa kwenye kongamano la kimataifa la kutokomeza polio lililopewa jina “kufikia hatua ya mwisho” (RLM) huko Abu Dhabi Falme za Kiarabu. Lengo kubwa la mkutano huo kwa mujibu wa WHO ni kusisitiza ahadi ya kutokomeza polio na fedha hizo ni kama awamu ya kwanza ya fedha zinazohitajika katika kutekeleza mkakati wa kimataifa wa kutokomeza polio wa mwaka 2019-2030.

Kongamano hilo la ahadi za kuchangia fedha limekuja wakati ambapo mwezi uliopita WHO ilitangaza kutokomezwa kwa aina mbili kati ya tatu za virusi vya polio na Zaidi ya hayo Nigeria nchi ya mwisho barani Afrika kuwa na visa vya polio haijashuhudia kisha chochote hadi sasa.

Ukanda mzima WHO Afrika unaweza kuthibitishwa kutokomeza kabisa virundi vya polio ifikapo 2020.

Akizungumza katika kongamano hhilo mkurugenzi mtendaji wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema “Kuzanzia kusaidia idadi kubwa kabisa ya wahudumu wa afya duniani, kumfikia kila mtoto kwa chanjo, mkakati wa kimataifa wa kutokomeza polio sio tu unatusogeza kuwa huru bila polio bali pia unajenga miundombinu ya muhimu ya kushughulikia mahitaji mengine ya afya. “

Ahadi zimetolewa wakati muafaka

Ameongeza kuwa “tunashuhuru ahadi zilizotolewa leo na pia tunazishukuru serikali, wahisani na washirika wetu kwa kusimama nasi. Hususan napenda kumshukuru mwana mfalme Sheikh Mohamed Bin Zayed Al Nahyan wa Abu Dhabi kwa kuwa mwenyeji wa kongamano hili ya kuchangisha fedha  na pia kwa msaada wake wa muda mrefu kwa ajili ya vita dhidi ya polio.”

Amesema huu ni wakati muhimu sana katika vita dhidi ya polio kwani kuna changamoto ya kumfikia kila mtoto ikiwemo kuwa na kampeni endelevu , kutokuwepo na usalama, vita, watu kuhamahama na katika wakati mwingine wazazi kukataa watoto wao kupewa chanjo kumesababisha kuendelea kuwepo kwa virusi vya polio katika nchi Pakistan na Afghanistan.

Ili kukabiliana na vikwazo vyote hivi na kuhakikisha watoto milioni 450 wanalindwa kila mwaka dhidi ya polio, serikali na wahisani wameahidi fedha hizo zitakazo piga jeki lengo la dola bilioni 3.27 zinazohitajika katika mkakati wa kutokomeza polio.