Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utekelezaji wa kanuani za AU umesaidia kutatua changamoto Afrika:El-Sisi

Rais wa Misri, Abdel Fattah El-Sisi akizungumza katika mjadala mkuu wa Baraza Kuu kikao cha 74 unaoendelea mjini New York, Marekani.
UN Photo/Cia Pak
Rais wa Misri, Abdel Fattah El-Sisi akizungumza katika mjadala mkuu wa Baraza Kuu kikao cha 74 unaoendelea mjini New York, Marekani.

Utekelezaji wa kanuani za AU umesaidia kutatua changamoto Afrika:El-Sisi

Masuala ya UM

Rais wa Misri, Abdel Fattah El-Sisi amesema mvutano unaoendelea  katika mazungumzo juu ya bwawa la Renaissance utakuwa na athari mbaya kuhusu utulivu na maendeleo katika eneo husika na nchini Misri kwa ujumla.

Akizungumza katika mjadala mkuu wa Baraza Kuu kikao cha 74 unaoendelea mjini Neyork kuhusu changamoto zilizopo nchi Misri katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGsBwana. El-sisi, amesema Maji ya mto Nile kwa Misri ni suala la uhai na maisha ambalo linaweka jukumu kubwa kwa jamii ya kimataifa kutekeleza na kusaidia kutatua changamoto hiyo, jukumu la kuwasihi wahusika wote kubadilika katika kusaka muafaka na kuridhia kwani athari za mto Nile zinakumba nchi nyingine nying za Afrika sio Misri pake yake.

El Sisi “ameonyesha utayari wa nchi yake kufikia makubaliano kwa masilahi ya kawaida ya watu wa wanaotumia mto wa Blue Nile huko Ethiopia, Sudan na Misiri."

Kwenye ngazi ya taifa , Sisi amesema nchi yake, chini ya uenyekiti wake wa Muungano wa Afrika (AU), imefanya kazi na wanajumuiya ili kujumuisha kanuni ya suluhisho la Kiafrika kwa shida za Kiafrika.

Na kuhusu Afrika kwa ujumla ili mpango mkamilifu wenye lengo la kuweka misingi ya maendeleo uweze kupitishwa ametaja hatua zinazochukuliwa ikiwemo uzinduzi wa Kituo cha Muungano wa Afrika cha Kulijenga upya bara hilo na Kuliendeleza, ambacho kitaangazia ujenzi wa nchibaada ya mizozo .

Rais Sisi amesema utekelezaji wa kanuni za kitaifa za umiliki rasililimali, na kwa kupitia jukumu kubwa la Muungano wa Afrika (AU, umesaidia kufikiwa makubaliano ya amani huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR na mtazamo wa pamoja kati ya vyama nchini Sudan na kusimamia kipindi cha mpito, akisisitiza umuhimu wa kuiondoa Sudan katika orodha ya wafadhili wa masuala ya ugaidi, "kwa kutambua mabadiliko mazuri yaliyoshuhudiwa na nchi hii ya kindugu ambayo ina uwezo wa kukabiliana na changamoto za kiuchumi kupitia mwingiliano na taasisi za uchumi za kimataifa ili kukidhi matarajio ya watu wake na kuchukua wajibu wake kama inavyostahili ndani ya jamii ya kimataifa.”

Rais huyo wa Misri amezitaka taasisi za kifedha za kimataifa, za bara na za kikanda kutimiza wajibu wao kikamilifu wa kufadhili maendeleo barani Afrika kwa njia bora na rahisi, akisema kwamba bara la Afrika ni bara la fursa ambazo zinaweza kuwa "jambo jipya kwa uchumi wa ulimwengu."