Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misri ni mshirika muhimu katika kuhakikisha amani na kazi za UN-Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres
UN
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres

Misri ni mshirika muhimu katika kuhakikisha amani na kazi za UN-Guterres

Amani na Usalama

Misri ni mshirika muhimu wa Umoja wa Mataifa na ina mchango mkubwa katika amani na usalama kwenye  ukanda huo na ushirikiano wetu na pia Misri ni muhimu katika kutekeleza kazi zetu za Umoja wa Mataifa.

Hayo ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akiwa mjini Cairo baada ya kukutana na rais Abdel Fattah el-Sisi ambapo wamejadili maswala mbali mbali yanayokabili ukanda huo ikiwemo Libya ambapo wakizungumza na waandishi wa habari kwa pamoja na waziri wa mambo ya nje katibu mkuu amesema

“Libya ilikuwa katikati ya mazungumzo yetu na lengo letu ni, kuhakikisha hakuna mizozo, kuweka mazingira kwa ajili ya kuimarisha usalama na muhimu ni kuzileta pamoja taasisi za Libya, bunge la Libya baraza la rais na  baraza la kitaifa la usalama.”

Guteress amesema hilo litawezekana kwa ushirikiano na wadau ili kuhakikuisha Libya inaungana na nchi zingine za kimataifa ili kuendesha taasisi zake vizuri na kurejesha uchumi wake na ushirikiano na jamii za kimataifa ambalo litakuwa na faida kwa ukanda mzima.

 Na kuhusu Palestina na Israeli bwana Guteress ameipongeza Misri kwa kazi ambayo imefanya hususan katika kuzuia ongezeko la uhasama Gaza,

 “dhamira ya Misri sio tu imezuia ongezeko la uhasama lakini imeruhusu uwasilishwaji wa misaada Gaza na mshikamano na Wapalestina pia ni muhimu na Umoja wa Mataifa unasimama pamoja na Misri katika juhudi hizo na nadhani tunakubaliana kwamba suluhu ni uwepo wa mataifa mawili ambapo Yerusalemitakuwa mji mkuukwa matiafa yote na kwetu sisi hakuna suluhu ya pili.”

Katibu Mkuu pia amesema wamezungumzia hali nchini Syria na Yemen ambako amesema kuhusu hayo wanamitzamo sawa. Aidha bwana Guterres amewaambia waandishi wa habari kuhusu suala la ugaidi ambako amesema kunapaswa kuwa na mbinu za kushughulikia wanachama wa vikundi vya kigaidi wanaokimbia mizozo na kwamba,

“dunia inapaswa kushirikiana katika kukabiliana na kutafuta suluhu na sio lazima kuuliza nchi ambazo ziko mstari wa mbele kugharamia na kukabiliana na athari za ugaidi.”

Katibu Mkuu amesema pia wamejadili ushirikiano wa mamlaka Misri na Umoja wa Mataifa unaongozwa na nguzo tatu za Umoja huo ambao ni amani na usalama, maendeleo endelvu na haki za binadamu.

Bwana Guterres ameshukuru watu na serikali ya Misri kwa ukarimu wao wakati wa ziara yake nchini humo na kwamba ametiwa moyo na uvumilivu na maarifa ya watu waMisri.