Kituo cha UN Women ni matumaini kwa wanawake wanaokimbia ukatili wa kijinsia Ethiopia

20 Machi 2019

Ukatili dhidi ya wanawake ni changamoto kubwa nchini Ethiopia na ili kuwanusuru wanawake na wasichana ambao maisha yao yameathirika na ukatili wa kingono, Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na maswala ya wanawake, UN Women kwa ushirikiano na serikali ya Denmark wameanzisha kituo salama kwa ajili ya wanawake wanaokabiliwa na ukatili wa kijinsia.

(Play Nats)

Hiyo ni sauti ya msichana aliyepewa jina Elina, ambaye kwa sasa  yupo katika kituo hicho salama, anasema, “baba yangu alimuua mama yangu, hiyo ni baada ya mama kugundua kwamba alikuwa ananifanyia ukatili wa kingono.

Kituo hicho kilichoko mji wa Adama nchini Ethiopia kimesaidia wanawake 680 na wasichana na watoto wao kujenga upya maisha yao na kuepukana na ukatili.

Kituoni hapo wanawake wanapewa makazi, huduma za tiba, msaada wa kisaikolojia na wa kisheria, elimu, mafunzo ya stadi za maisha na mbinu za kujikinga. Kituo hicho kinashirikiana na polisi na kutoa mafunzo kwao kuhusu namna ya kushuhgulikia kesi zinazohusiana na ukatili wa kingono.Sintayehu Botela ni inspekta wa polisi mjini Adama

(Sauti ya Botela )

«Tunashirikiana na nyumba salama, wanatupa mafunzo kuhusu kuwalinda wanawake na wasichana, iwapo mtu anafanya makosa tunahakikisha kwamba anashtakiwa, tunatoa mafunzo pia kwa jamii kuhusu jinsi ya kuwalinda wanawake na wasichana .”

Kituo hiki kinatoa fursa kwa wanawake kujitegemea na kuwa jasiri katika maisha ya baadaye na hivyo kuwawezesha kusongea kufikia ndoto zao kama anavyosema Elina.

(Sauti ya Elina)

“Lengo langu ni kuwa daktari ili niweze kuwasaidi watu wengine, hususan watu waliopitia changamoto kama mimi, niña matumaini ya kuwasaidia.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter