Skip to main content

Matumaini ya waathirika wa ukatili wa kingono DRC yafufuliwa:MONUSCO

Wanawake waliopitia ukatili wa kingono. Picha: UM

Matumaini ya waathirika wa ukatili wa kingono DRC yafufuliwa:MONUSCO

Masuala ya UM

Katika jitidaha za kupambana na unyanyasaji na ukatili wa kingono katika maeneo ya operesheni za Umoja wa Mataifa hasa kuliko na vita , Umoja wa Mataifa umelivalia njuga suala hilo na kuwasaidia waathirika kwa kuzindua mirandi mbalimbali itakayowasaidia.

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ujulikanao kama MONUSCO uko mstari wa mbele na wiki hii umezindua rasmi miradi huo mjini Sake Goma, jimbo la Kivu ya Kaskazini.

Lengo kubwa ikiwa ni kuimarisha jamii kupitia mafunzo ya vijana na wanawake walioathirika na unyanyasaji na ukatili wa kingono lakini pia ukatili wa aina nyingine, na kisha kuwapa fursa ambazo zitawaepusha kujihusisha na biashara ya ngono.

Miradi hiyo ambayo inahusisha pia mashirika ya kijamii na wanaharakati itasaidia kuwajumuisha waathirika katika mazingira yao ya nyumbani. Faustine Kasore ni Rais wa kamati ya mtandao wa kuwasilisha malalamiko (CBN) jimboni Kivu Kaskazini anasema mradi huo umekuja wakati muafaka

(SAUT YA FAUTINE KASORE)

Kwani amesema

(SAUTI YA FAUSTINE KASORE)

Zaidi ya watu 500 wananufaika kwa kujifunza biashara, kuzalisha chakula na kujiongezea kipato. Miradi hiyo inafadhiliwa na mfuko maalumu kwa ajili ya waathirika wa unyanyasaji na ukatili wa kingono  kwa gharama ya dola 175,000, na michango mingine kutoka serikali ya Japan na Norway na majimbo yote mawili ya Kivu Kaskazini na Kusini yanashirikishwa.

Kwa mujibu wa MONUSCO miradi hiyo ni sehemu ya jitihada za Umoja wa Mataifa kukomesha ukatili wa kingono kila mahali palipo na operesheni zake na sasa maandalizi yanafanyika kwa ajili ya uzinduzi wa miradi kama hiyo Liberia na Jamhuri ya afrika ya Kati CAR.