Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya vifo kufuatia tetemeko Indonesia sasa zaidi ya 2000

Timu ya taifa ya uokoaji nchini Indonesia wakiopoa maiti kwenye kifusi baada ya jengo kusambaratisha na tetemeko la ardhi Sulawesi mwezi Septemba 2018
Picha na (BNPB), Indonesia.
Timu ya taifa ya uokoaji nchini Indonesia wakiopoa maiti kwenye kifusi baada ya jengo kusambaratisha na tetemeko la ardhi Sulawesi mwezi Septemba 2018

Idadi ya vifo kufuatia tetemeko Indonesia sasa zaidi ya 2000

Tabianchi na mazingira

Idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko la ardhi nchini Indonesia inaendelea kuongezeka na sasa ni zaidi ya 2,000, umesema Umoja wa Mataifa ambao unanuia kuwasaidia waathirika karibu 200, 000 kupitia juhudi zinazoongozwa na serikali.

Kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa tetemeko hilo la tarehe 28 Septemba lililoandamana na tsunami nchini Indonesia, hadi sasa vifo vimefikia 2,010, na majeruhi 10,700, huku watu 700 hawajulikani walipo.

Mashirika yanayoisaidia juhudi zinazoongozwa na serikali ya Indonesia, yanalenga kusaidia watu 191,000 walioko kwenye hali mbaya wasiokuwa na makao, chakula, maji safi na bila huduma zingine za msingi.

Mara baada ya maafa ya tetemeko la ardhi na tsunami kutokea, watoaji huduma walianza juhudi za kuoka watu waliokwama kwenye vifusi vya majengo na kutoa huduma ya kwanza kwa waathirika.

Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya  Kibinadamuna misaada ya dharura  (OCHA), juhudi kadhaa zinafanywa kuwafikia watu waishio kwenye maeneo yaliyoathirika. Watoaji huduma ya misaada ya kibinadamu wa mashirika mbalimbali ikiwa  ni pamoja na Umoja wa Mataifa, mashirika ya kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali, shirika la msalaba mwekundu la Indonesia na serikali ya Indonesia, wanajitahidi kadri iwezekanavyo kusaidia maeneno yaliyoaathirika zaidi.

Zaidi ya nyumba 67,000 zimeharibiwa ama kusambaratishwa kabisa na tetemeko la ardhi, tsunami au mmomonyoko wa udongo, na kuacha watu 333,000 bila makazi. Watu 62,400 wamelazimika kuhama makwao kwa sababu ya majanga hayo na sasa wanaishi kwenye makazi ya muda mfupi bila huduma za msingi. Kwa mujibu wa shirika la kitaifa la kudhibiti majanga (BNPB), zaidi ya shule 2,700 zimeharibiwa, pamoja na vituo 20 vya afya na mifumo ya maji.

Kusaidia mahitaji muhimu, shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM litatoa galoni 28,000 za maji ya chupa na makazi 1,700 ya dharura. Shirika la chakula dunani WFP, nalolimeweka ghala la hifadhi ya chakula  muda mfupi kwa ajili usimamizi bora.

Kwa kuwa watoto na wanawake ndio waathirika wakubwa baada ya kutokea majanga kutokea huduma za ulinzi zimeandaliwa  ikiwa ni pamoja na juhudi  zinazoongozwa za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kuwaunganisha tena na familia zao  watoto waliopotea. Mahema ya matibabu ya dharura yamewekwa na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani, UNFPA ili kutoa huduma za uzazi. Vitengo vya usafi na uzazi navyo vimegawanywa na timu ya wakunga imewasili.

Muda mfupi baada ya maafa hayo, OCHA lilitenga dola za kimarekani milioni 15 kusaidia shughuli mbalimbali za kibinadamu, hususan kwenye maeneo yaliyopanga mipango ya dharura kwa ushirikiano wa Umoja wa mataifa na serikali ya Indonesia. Mpango huo unahitaji dola za kimarekani milioni 50.5 ili kusaidia watu 191,000 hususan wanawake, watoto na wanaume walioathiriwa zaidi.