Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hofu yatanda huku juhudi zikifanyika kwa waathirika wa tetemeko Indonesia:UN

Tarehe 30 Septemba 2018, wakazi nchini Indonesia wakiondoa maiti waliopoteza maisha kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililopiga eneo la Palu katika hifadhi ya taifa ya Balaroa, jimbo la Sulawesi kati. Tetemeko na tsunami vilipiga 28/9/2018
© UNICEF/Arimacs Wilander
Tarehe 30 Septemba 2018, wakazi nchini Indonesia wakiondoa maiti waliopoteza maisha kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililopiga eneo la Palu katika hifadhi ya taifa ya Balaroa, jimbo la Sulawesi kati. Tetemeko na tsunami vilipiga 28/9/2018

Hofu yatanda huku juhudi zikifanyika kwa waathirika wa tetemeko Indonesia:UN

Msaada wa Kibinadamu

Ikiwa ni siku nne tangu kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi na tsunami kwenye kisiwa cha Sulawesi nchini Indonea, Mashirika ya Umoja wa Mataifa  na washirika wao wameonya kwamba baadhi ya jamii zilizoathirika bado hazijafikiwa na msaada wowote huku idadi ya waliopoteza Maisha ikitarajiwa kuongezeka.

Hadi kufikia leo  “Serikali ya Indonesia imethibitisha kwamba watu 1,234  wamepoteza maisha kufuatia zahma hiyo Sulawesi,” Jens Laerke,ni msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA, mjini Geneva.

“Takriban watu 800 people wamejeruhiwa vibaya na wengine karibu 100 bado hawajulikani waliko. Kuna uwezekano mkubwa idadi ya vifo na majeruhi ikaongezeka wakati maeneo mengi yanaanza kufikiwa na wakati serikali ikiendelea na tathimini zaidi.”

Mamia ya watu wameripotiwa kufariki dunia kutokana na tetemeko la ardhi na tsunami huko Sulawesi nchini Indonesia tarehe 28 Septemba 2018
© UNICEF/Arimacs Wilander
Mamia ya watu wameripotiwa kufariki dunia kutokana na tetemeko la ardhi na tsunami huko Sulawesi nchini Indonesia tarehe 28 Septemba 2018

Katika wilaya ya Sigi Biromaru mjini Palu kanisa lililoporomoka na kusambaratika kabisa wahudumu wa uokozi wameelezea hali iliyoghubikwa na changamoto kubwa  wakijaribu kujikita kwenye tope zito ili kuweza kuopoa maiti za vijana zaidi ya 30 waliokuwa kwenye mafundishi ya kusoma Biblia tetemeko lilipozuka.

Matthew Cochrane msemaji wa shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu (IFRC) akifafanua kuhusu hilo amesema “ Iliwachukua saa moja na nusu kubeba maiti moja moja na kuzipeleka kwenye gari ya kubebea wagonjkwa baada ya kuzama kwenye tope kuziopoa.”

Ameongeza kuwa “Hali ya wanaofanya shughuli hiyo ni ya kuchanganyikiwa, na  bado kuna eneo kubwa na mahali ambapo huenda ndipo palipoathirika zaidi bado lhalijafikiwa, lakini timu zinaendelea kung’ang’ana na kufanya kila wawezalo.”

Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wake tayari yameitikia wito wa serikali ya Indonesia wa msaada, lakini fursa ya kufika kila palipoathirika ndio mtihani mkubwa hususan maeneo ya pwani na katikati mwa Sulawesi ambako kiwango cha uharibifu bado hakijajulikana.

Baada ya tetemeko wakazi wakiangalia kiwango cha uharibifu na kilichosalia kufuatia tetemeko na tsunami vilivyopiga eneo la Sulawesi kati nchini Indonesia tarehe 28 mwezi Septemba mwaka huu wa 2018
© UNICEF/Arimacs Wilander
Baada ya tetemeko wakazi wakiangalia kiwango cha uharibifu na kilichosalia kufuatia tetemeko na tsunami vilivyopiga eneo la Sulawesi kati nchini Indonesia tarehe 28 mwezi Septemba mwaka huu wa 2018

Kama sehemu ya msaada wa kimataifa , shirika la mpango wa chakula duniani WFP limethibitisha kwamba linawasiliana kwa karibu na serikali tangu Ijumaa iliyopita lilipotokea tetemeko hilo  na ghala la WFP laililopo Subang, Malaysia, liko tayari kutoa msaada wa dharura kwa mujibu wa msemaji wa shirika hilo Herve Verhoosel

“Maafisa wa masuala ya kiufundi wa WFP wamewasili Sulawesi na msafara wa serikali na wanatoa ushauri kwa serikali kuhusu masuala ya kiufundi katika operesheni zinazoendelea. Hali ni ngumu kukiwa na upungufu mkubwa wa mafuta, barabara zimeharibiwa, miundombinu ya bahari na viwanja vya ndege inaathiri utendaji na hakuna mawasiliano.”

Athari ya zahma hiyo kwa watoto ndio inayotia hofu kubwa limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF huku tayari zaidi ya asilimia 40 ya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano katikati mwa kisiwa cha Sulawesi wana matatizo ya kudumaa kutokana na utapia mlo.

 

Mkazi mmoja akihamisha angalau mabaki ya vifaa vyake vilivyosalia kwenye nyumba yake iliyosambaratishwa na tetemeko la ardhi huko Indonesia tarehe 28 mwezi uliopita wa Septemba 2018
© UNICEF/Tirto.id/@Arimacswilander
Mkazi mmoja akihamisha angalau mabaki ya vifaa vyake vilivyosalia kwenye nyumba yake iliyosambaratishwa na tetemeko la ardhi huko Indonesia tarehe 28 mwezi uliopita wa Septemba 2018

Kwa mujibu wa msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, Christophe Boulierac ukweli kwamba asilimia 33 pekee ya watoto wote waliozaliwa kwenye eneo hilo ndio walioandikishwa inaweza kuwa changamoto kubwa katika juhudi za kuwaunganisha watoto waliosalia peke yao na familia zao.

“Tuna hofu kuhusu tunachookifahamu kkwa mantiki ya athari kwa watoto, lakini lakini ni kile tusichokijua bado wakati taarifa za ukubwa wa janga hili zikiendelea kuibuka, na katikati ya Suwalesi hofu yetu sio tu usalama kwa watoto mjini Palu lakini pia katika mji wa Dongala na jamii zingine ambazo bado zimekatwa na mawasiliano na msaada wa kibinadamu.”

Kipaumbele cha msingi hivi sasa kwa serikali ni pamoja na kuwahamisha watu kutoa maeneo yaliyoathirika Zaidi limesema shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM, lakini usafiri unasalia lkuwa changamoto na barabara nyingi zimesambaratishwa kabisa.

Mapema leo mkuu wa ofisi ya IOM Indonesia Mark Getchell, alijadili hali hiyo na serikali ya Indonesia na kuongeza kuwa misaada inaweza kufikishwa kwa njia ya daraja la kibinadamu kutoka Jakarta hadi Sulawesi, mkakati ambao ulitumika pia baada ya zahma ya tsunami ya 2004 kwenye bahari ya Hindi fkutoka Jakarta to Aceh na kutoka Medan hadi Aceh.

Magari yaliyo rundikana na mengine kupondeka   babada ya kusombwa na maji na Tsunami katika baech ya Talise, Palubaada ya tetemeko la ardhi lililokumba Sulawesi Septemba 28.
© UNICEF/Arimacs Wilander
Magari yaliyo rundikana na mengine kupondeka babada ya kusombwa na maji na Tsunami katika baech ya Talise, Palubaada ya tetemeko la ardhi lililokumba Sulawesi Septemba 28.

Kwa mujibu wa msemaji wa IOM Dilon kupeleka misaada Sulawesi kupitia bandari ya Palu inaendelea kuwa changamoto kubwa lakini “Bandari yenyewe haijaharibika lakini mitambo yake ambayo inatumika kubebda na kuhamisha mizigo na kuingiza melini imeharibika vibaya  na katika baadhi ya maeneo imesambaratishwa kabisa n ahata kuingia bandarini kwenyewe ni shida.”

Ingawa kipaymbele ni kuwafikia manusura, lakini uharibufu katika moundombinu ya msingi, na ukosefu wa maji safi vinatoa tishio kubwa la kiafya.

Hata kabla ya janga hili, Donggala na Palu kulikuwa na visa vya ugonjwa wa kuhara na maradhi ya mfumo wa hewa amesema Tarik Jasarevic, ambaye ni msemaji wa shirika la afya duniani (WHO). Ameongeza kuwa

“Ambacho tutakishuhudia kama ilivyo kila wakati katika hali kama hizi ni majeruhi zaidi ya wale ambao tayari wamesharipotiwa kama tayari ni zahma ya kiafyahe.bila shaka ukosefu wa malazi na maji na huduma za usafi kunaweza kuzusha mlipuko wa kuhara na magonjwa mengine ya kuambukiza.”

Maafisa wa WHO wamesema tathimini ya awali iliyofanywa na maafisa wa Indonesia inaonyesha hospital moja imeharibiwa na zingine bado zinafanyiwa tathimini. Kwa ushirikiano na wizara ya afya kitengo cha dharura , WHO pia inajiandaa kujitolea kupeleka timu ya wataalamu wa afya.