UNFPA

Mchakato wa amani unaojumuisha wanawake ni kitovu cha amani endelevu Afghanistan- Bi. Mohammed

Chonde chonde wananchi wa Afghanistan fikieni maridhiano ya yaliyopita na muwajumuishe wanawake kwenye harakati zote za mchakato wa amani ya kudumu na sauti zao kwenye mchakato wa kisiasa zisikike, amesema Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed.

UN yataka nchi kuzingatia uwiano kati ya idadi ya watu na maendeleo

Wakati idadi ya watu duniani ikikadiriwa kuongezeka na kufikia bilioni 9 mwaka 2050 Umoja wa Mataifa imezitaka nchi kuzingatia uwiano kati ya ongezeko la idadi ya watu na maendeleo

Sauti -
2'39"

Wakati wa kuchukua hatua ni sasa wanawake na wasichana hawawezi kusubiri haki zao:UN

Wakati idadi ya watu duniani ikikadiriwa kuongezeka na kufikia bilioni 9 mwaka 2050 Umoja wa Mataifa imezitaka nchi kuzingatia uwiano kati ya ongezeko la idadi ya watu na maendeleo

Waathirika wa kimbunga Idai wawezeshwa na UNFPA Msumbiji

Umoja wa Mataifa kupitia shirika la Idadi ya watu duniani UNFPA wamekuwa na jukumu kubwa la kuwezesha wanawake mashinani kujikwamua siotu na umasikini bali  katika masuala ya kiafya ikiwa ni pamoja  afya ya uzazi, kupiga vita ukatili wa kijisnia na pia ushauri nasaha kwa waathirika wa magonjwa mb

Sauti -
4'22"

Genge la watu kumbaka mtoto wa miaka 9 ni unyama usiostahili:UNFPA

Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA leo limelaani vikali unyama na ukatili uliofanywa na genge la watu nchini Somalia wa kumbaka binti wa miaka 9 .

27 Mei 2019

Ikiwa leo ni siku ya mapumziko nchini Marekani ambapo inasherehekewa siku ya kuwakumbuka mashujaa, tunakuletea jarida maalumu kuhusu ugonjwa wa Fistula. Utawasikia wagonjwa na pia madaktari. Elimika.

Sauti -
9'53"

Bado Fistula ni tishio kwa wanawake wanaojifungua, hatua zaidi zahitajika- UNFPA

Licha ya tahadhari na jitihada kubwa zinazofanyika kote duniani kuwanusuru , ugonjwa wa Fistula umeendelea kuwa ni jinamizi linalowaghubika kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA. Flora Nducha na taarifa kamili

Sauti -
1'56"

22 Mei 2019

Je wajua kampuni zenye viongozi wa ngazi ya  juu wanawake na wanaume hupata faida zaidi? Basi fuatana nani katika utafiti wa shirika la kazi duniani, ILO. Tunamulika pia masuala ya fistula ambapo licha ya  hatua zilizochukuliwa bado fistula ni jinamizi linalogubika wanawake.

Sauti -
11'51"

Idadi kubwa ya wanawake hawana sauti ya maamuzi kuhusu miili yao-UNFPA

Haki za afya ya uzazi na chaguo ni jambo la uhalisi kwa wanawake wengi sasa kuliko wakati mwingine wowote kwa mujibu wa ripoti ya shirika la umoja wa mataifa la idadi ya watu, UNFPA kuhusu hali ya idadi ya watu duniani mwaka 2019 iliyotolewa leo Jumatano.

Sauti -
4'44"

10 Aprili 2019

Idadi kubwa ya wanawake bado hawana sauti ya maamuzi kuhusu miili yao yasema ripoti ya UNFPA.  Nayo ripoti ya UNICEF yashauri, ukitaka ushindani katika uchumi kesho, wekeza leo katika katika elimu ya awali ya watoto.

Sauti -
11'56"