Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasambaza msaada kwa waathirika wa tsunami Indonesia

IOM yasambaza msaada kwa waathirika wa tsunami Indonesia

Shirika la kimataifa la Uhamiaji IOM limepeleka zaidi ya tani 1400 za chakula na midaada mingine kwa niaba ya serikali ya Indonesia katika maeneo ya vijijini yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi pamoja na Tsunami mwezi Oktoba mwaka uliopita.

Janga hilo lililosababisha vifo vya watu 509 pia lilisababisha zaidi ya watu 11,000 kupoteza makao na kuharibu vijiji pwani ya kisiwa cha Sumatra.

Hata hivyo shughuli ya usafirishaji wa misaada inakabiliwa na chamgamoto zikiwemo barabara mbaya katika visiwa hivyo .IOM inasema kuwa itatumia mashua ndogo kusafirisha chakula kwenda kwa maeneo ambayo ni vigumu kufikika kwa njia ya barabara.