Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

DRC yaridhia chanjo za majaribio kwa wagonjwa wa Ebola

Sampuli za damu zinachunguzwa katika maabara maalum mjini Mbandaka, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Picha ya WHO/Oka
Sampuli za damu zinachunguzwa katika maabara maalum mjini Mbandaka, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

DRC yaridhia chanjo za majaribio kwa wagonjwa wa Ebola

Afya

Ebola! Sasa wagonjwa DRC  kuulizwa ridhaa yao iwapo wanataka wapatiwe chanjo ya majaribio dhidi ya ugonjwa huo.

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC imerithia wagonjwa wa Ebola kwenye jimbo la Equateur nchini  humo wapatiwe matibabu kwa kutumia aina tano za dawa ambazo bado ziko kwenye uchunguzi.

 

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limesema uamuzi wa kumpatia mgonjwa tiba kwa kutumia dawa hizo utafanywa na daktari kwa kuzingatia hali ya kiafya ya mgonjwa na ridhaa ya mgonjwa.

 

Hii ni mara ya kwanza kwa tiba ya aina hiyo kuruhusiwa katikatiya mlipuko wa Ebola.

 

Chanjo za Ebola zikiandaliwa tayari kupatiwa wakazi wa Mbandaka huko jimboni Equateur nchini DRC.
WHO/Oka
Chanjo za Ebola zikiandaliwa tayari kupatiwa wakazi wa Mbandaka huko jimboni Equateur nchini DRC.

WHO inasema watoa huduma katika kliniki zinazotibu Ebola kwenye maeneo ya Bikoro, Iboko na Mbandaka kwenye jimbo la Equateur nchini humo wataamua ni dawa gani inafaa kusaidia mgonjwa na pia watazingatia mazingira waliyomo.

 

Pamoja na kupata ridhaa ya mgonjwa, lazima taratibu za utoaji wa dawa hizo zizingatiwe , huku mgonjwa akifuatiliwa kwa karibu baada ya kupatiwa tiba hiyo.

 

Dawa nne kati ya tano zilizopo nchini DRC na ambazo zimeidhinishwa kutumika ni

Zmapp, GS-5734, REGN na mAb114.

 

Hadi leo hii madaktari wasio na mpaka, MSF wanashirikiana na serikali ya DRC kutoka chanjo dhidi ya ebola huko Bikoro na Iboko ilhali WHO inasaidia katika mji wa Mbandaka.

 

Miji hiyo ni ambako Ebola imethibitishwa kuwepo tangu kutangazwa rasmi kwa mgonjwa mwezi Mei na hadi sasa visa vilivyoripotiwa ni 57.

 

TAGS: Ebola, chanjo, DRC, Mbandaka, Iboko, Bikoro, Equateur