UN yajipanga kuzuia usafirishaji binadamu angani

5 Januari 2018

Biashara haramu ya kusafirisha binadamu kwa ajili ya utumikishwaji inashika namba tatu baada ya usafrishaji wa madawa na silaha duniani.

Umoja wa mataifa kupitia 0fisi yake ya Haki za binadamu kwa kushirikiana na wadau wa usafirishaji wa anga duniani wamebuni muongozo maalum ambao unaelezea mafunzo maalum kwa wahudumu ndani ya ndege ili kuweza kubaini abiria wanaokuwa wanasafirisha isivyo kihalali.

Youda Hadaddin ni mshauri kuhusu usafirishaj haramu wa binadamu  kutoka ofisi ya haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa amesema ijapokuwa vado mpango huo haujazidnuliwa rasmi lakini  baadhia ya mamlaka za ndege zimeshaanza kutekeleza miongozo ya kufundidha ambapo Canada imekwisha tengeneza mtaala huku Marekani imeanza kutoa mafunzo katika vyuo vyake

(Sauti ya Youda Hadaddin)

“Sisi abiria tunapokuwa angani, wahudumu wa ndege wanatuona na kutusoma tabia zetu na mienendo yetu na watu tulioongozana nao. Na hivyo wanaweza kuhisi kitu, na kama wana wasiwasi wawashirikishe wafanyakazi wenzao. Bila shaka jambo muhimu wanalopaswa kuzingatia ni kwamba wasimdhuru mtu yeyote. Hawapaswi kuingilia kumuokoa mtu au hata kuonyesha abiria wengine kuwa pale pana tatizo. Wanakusanya taarifa zote halafu wanawasilisha kwa rubani ambaye ndiye msimamizi mkuu. Rubani atawasilisha taarifa hizo kwa wafanyakazi na polisi wa uwanja wa ndege, na jukumu lao linaishia hapo.”

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni zaidi ya watu milioni 41 wanasafirishwa isivyo kihalali na asilimia 52 kati yao ni wanawake.

Mwongozo huo utazinduliwa mwezi Machi mwaka huu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud