Saudi Arabia yakandamiza haki za banadamu
Saudi Arabia inaendelea kutumia sera na sheria zake kuhusu masuala ya usalama na ugaidi kukandamiza wanaoipinga serikali.
Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa leo na jopo la wataalamu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa huko Geneva Uswisi
Wataalamu hao wamesema viongozi wa dini, wanaharakati, wapinzani, waandishi wa habari na yeyote anayeipinga serikali nchini Saudi Arabia amejikuta akishikiliwa na vyombo vya dola na kuhukumiwa ambapo tangu mwezi Septemba mwaka 2017 zaidi ya watu 60 wamekamatwa.
Jopo limesema haki ya uhuru wa kujieleza na kutoa maoni inabanwa sana Saudi Arabia.
Wataalamu hao wameitaka Saudi Arabia kutekeleza maazimio mawili yaliyotolewa na Umoja wa Mataifa kwa kuzingatia mkataba wa haki za binadamu uliosainiwa na nchi hiyo.