Skip to main content

Ahadi yetu Colombia ipo palepale:Guterres

katibu mkuu Antonio Guterres akihutubia kwenye mkutano wa waandishi wa habari katika ikulu  nchini Colombia

Ahadi yetu Colombia ipo palepale:Guterres

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres yupo ziarani nchi  Colombia, Amerika kusini katika jitihada za kuendeleza mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Colombia na makundi ya waasi nchini humo.

Katika ziara yake ya kwanza kabisa tangu achukue wadhifa ya ukatibu mkuu wa Umoja wa Mataifa,Bw. Guterres alipokelewa na rais wa Colombia Bw. Juan Manuel Santos na kuongea na vyombo vya habari huko Casa de Nariñ ikulu ya colombia ambapo bwana Guterres ameipongeza serikali ya Colombia kwa jitihada za kukaa meza moja na waasi wa FARC ikiwa ni hatua ya kutafuta amani ya kudumu na pia ushirikiswaji wa pande zote kinzani katika ujenzi wa taifa la Colombia. Bwana Guterres amesema

Sauti ya Antonio Guterres

Hivi sasa, tunshuhudia migogoro mipya kote duniani, na migongano ya zamani inaonekana kutopatiwa ufumbuzi. Kwa mantiki hiyo kilichotokea Colombia ni mfano wa kuigwa na ulimwengu. Ninaamini kwamba ni wajibu wa jamii ya kimataifa kutoa ushirikiano kikamilifu katika mchakato wa kujenga amani nchini Colombia.

Na kuhusu hatua zipi zilizochukuliwa na Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha amani colombia ni ya kudumu bwana Guterres alisema…

Sauti ya Antonio Guterres

Swala sio tu juu ya kujenga amani lakini kuhakikisha uwepo wa Serikali moja katika taifa lote la Colombia. Uwepo wa utawala, usalama, huduma za umma, elimu, afya, maendeleo. Ni changamoto kubwa, ni jambo lisilofanyika kwa muujiza, lakini nataka kurudia ahadi ya Umoja wa Mataifa ya kusaida serikali ya Colombia katika mchakato huu mkubwa wa ujenzi wa amani lakini wakati huo huo kujenga demokrasia ya umoja.