ICTY ilikuwa mfano- Baraza

1 Januari 2018
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa wamezungumzia hitimisho la mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita kwa iliyokuwa Jamhuri ya Yugoslavia ICTY hii leo tarehe 31 Desemba 2017.

Katika taarifa yao, wajumbe wamerejelea azimio namna 827 la mwaka 1993 la kuundwa kwa mahakama hiyo iliyopatiwa jukumu la kusimamia mashitaka na pia kuhukumu wahalifu wa kivita huko Yugoslavia.

 Ikumbukwe tu kwamba uundwaji wa ICTY, iliyomhukumu aliyekuwa mkuu wa jeshi la Bosnia Ratko Mladić, ilianzishwa katika misingi ya mfano wa mahakama a Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ("ICTR"), kama ilivyoelezwa katika Sheria ya kimataifa ya haki za binadamu.

 Wajumbe wa Baraza la Usalama wanasisitiza uamuzi wao wa kuendelea kupambana na wote wanaohusika na makosa ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu na sheria za kimataifa za uhalifu wa kivita, pia wameomba ushirikiano na vyombo vya usalama vya mataifa yote duniani kutekeleza wajibu wao wa kusimamia haki na sheria na pia kuwafikisha watuhumiwa katika mahakama husika ilI sheria ichukue mkondo wake.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter