Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi walioko Uganda wazungumzia krismasi yao

Nchini Uganda, wakimbizi kutoka Sudan Kusini na DRC wakiwa katika harakati za kupata mlo. (Picha:UN/Mark Garten)

Wakimbizi walioko Uganda wazungumzia krismasi yao

Nchini Uganda, maelfu ya wakimbizi kutoka nchi jirani za Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wamesaka hifadhi kutokana na machafuko nchini mwao. Je kwao wao sikukuu ya Krismasi iko vipi? Ungana basi na Joseph Msami kwenye jarida hili maalum ambalo kwamo John Kibego amevinjari kwenye kambi ya wakimbizi ya Kyangwali nchini Uganda.