Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki ya Kulinda ni jukumu la kila mtu:Migiro

Haki ya Kulinda ni jukumu la kila mtu:Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Asha Rose Migiro katika kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya Rwanda amesema wakati dunia ikiwakumbuka waliopoteza maisha katika mauaji hayo na walionusurika ni lazima kuendelea na kazi ya kuhakikisha haki inapatikana, kuchagiza amani na upatanisho na kuzuia mauaji ya kimbari na uhalifu kama ho ktokea tena popote duniani.

Ameongeza kuwa kumbukumbu ya leo ni kumbusho kwamba juhudi za pamoja zinahitajika katika kutambua daliliza za onyo la kuzuka kwa ghasia. Amesema juhudi za serikali na wananchi wa Rwanda zinatambulika na wengine wote wanaoisaidia nchi hiyo kurejea katika maisha ya kawaida baada ya janga hilo.

Mmoja wa manusura wa mauaji hayo kutoka Rwanda ni Jean Marie Kalisa anasema umefika wakati wa kusahau yalopita na kuganga yajayo kwa Wanyarwanda wote, Watutsi na Wahutu.

(SAUTI YA JEAN MARIE KALISA)