Mkutano wa maandalizi kuhusu uhamiaji salama wang’oa nanga Mexico
Mkutano wa maandalizi kuhusu makubaliano ya kimataifa yanaozingatia uhamiaji salama na wa haki , umeanza hi leo hadi tarehe 06 Desema , katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa mjini Puerto Vallarta Mexico.
Mkutano huo ulioleta pamoja washiriki mbalimbali zikiwemo serikali, asasi za kiraia , Umoja wa Mataifa na mashirika binafsi lengo lake ni kutoa jukwaa kwa nchi mbalimbali na wadau kujumika na kutoka na mtazamo wa pamoja kwa ajili ya uhamiaji salama na stahuiki.
Mkutano huo ulioratibiwa na serikali ya Uswis na mwenyeji serikali ya Mexico chini ya usimamizi wa rais , Enrique Pnea unafanyika kwa mujibu wa azimio la Umoja wa Mataifa nambari 71/280 linalohimiza mkutano kuhusu makubaliano ya kimataifa ya uhamiaji kufanyika katika awamu tatu ambapo awamu ya kwanza kuhusu mashauriano ulifanyinka kati ya mwezi April na Novemba mwaka huu , awamu ya pili kuhusu uhifadhi kati ya Novemba na Januari na awamu ya tatu na ya mwisho kuhusu mazungumzo baina ya serikali utafanyika kati ya Februari na Juni mwaka 2018.
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhamiaji Bi Louis Arbour, akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo amesema licha ya kauli ya rais wa marekani Donald Trump ya kuonyesha dalili ya kuiondoa nchi yake katika muungano wa mjadala wa uhamiaji, bado kuna matumaini kwamba sehemu kubwa ya Marekani inaunga mkono mjadala wa uhamiaji salama na wa haki. Ameongeza kuwa
(Sauti ya Louise Arbour)
Kuna haina nyingi na tofauti ambazo zinatomika katika utekelezaji wa uhamiaji, moja wapo ni kwamba watu huhamia moja kwa moja, wengine huhamia kwa muda wakiwa na nia ya kurudi makwao. Swala linakuja kwamba tukiamua kuliongelea swala la uhamiaji ni lazima hamasa iwe ya kimataifa kwa mlengo wa eneo husika. Na hii ni nafasi ya kipeke kwa nchi wanachama kuongelea matarajio yako katika mkutano ujao. Na ni katika mkutano huo ambapo azimio kuhusu uhamiaji salama na wa haki utazungumziwa.