Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wapongeza hukumu dhidi ya Mladic

Mahakama ya kimataifa ya Jinai ya Yugoslavia ya zamani ICTY. Picha: ICTY

Umoja wa Mataifa wapongeza hukumu dhidi ya Mladic

Kamishina mkuu wa haki za binadam wa Umoja wa Mataifa amekaribisha hukumu iliotolewa leo dhidi ya aliyekuwa kamanda wa jeshi la Wasebia nchini Bosinia, Ratko Mladic, ambayo imetolewa na mahakama ya kimataifa ya Jinai ya Yugoslavia ya zamani ICTY, kuhusiana na mashitaka lukuki ya mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.

Bwana Zeid Ra’ad Al Hussein ametaja hukumu dhidi ya Mladic kuwa ni ushindi mkubwa wa kisheria na haki.

image
. Picha: ICTY
Madic alikuwa ni mshukiwa mkuu wa baadhi ya makosa makubwa ya uhalifu  barani Ulaya tangu vita ya pili ya dunia, yakiwemo kuanzisha ugaidi, mauaji  dhidi ya maelfu ya wanaume na wavulana wa Kiislam na uharibifu, majanga na athari za kisaikolojia kwa watu wengine wengi zaidi.

Hukumu hiyo imetoana na juhudi za wahanga na mashahidi ambao walisalia na matumaini kwamba siku moja angefikishwa mbele ya mahakama, amesema Kamishina Mkuu, Zeid ambaye alihudumu Yugoslavia ya zamani chini ya kikosi cha jeshi la Umoja wa Mataifa kati ya 1994 na 1996.

Madic ambaye amehukumiwa kwenda jela Maisha  ni mtu wa pili kupatiwa hukumu ya kifungo kirefu, miongoni mwa waliopanga ukatili mkubwa zaidi Bosnia na Herzegovina. Wa kwanza alikuwa ni Radovan Karadzic.

Hivyo Zeid amesema hukumu  hii iwe onyo kwa watekelezaji wa uhalifu dhidi ya ubinadamu kama huo na kwmaba hawatawahi kukwepa sheria, hata wawe wa tabaka ya juu zaidi au ichukuwe muda mrefu kiasi gani.