Zanzibar na harakati za kulinda mazingira ili kuchagia utalii

20 Novemba 2017

Huko visiwani Zanzibar nchini Tanzania, uharibifu wa mazingira hususan maeneo ya baharini unatishia mustakhbali wa utalii ambao ni moja ya vyanzo vikuu vya mapato visiwani humo. Katika mkutano wa hivi karibuni wa tume ya Umoja wa Mataifa kwa uchumi wa Afrika, ECA huko Comoro ambako washiriki kutoka serikali walipazia fursa na vikwazo vya uchumi. Miongoni mwao ni Aboud Jumbe ambaye ni mkuu wa utafiti na mipango, Idara ya Mazingira kwenye wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Bwana Jumbe katika mahojiano na Priscilla Lecomte wa ECA, kutoka Kigali, Rwanda aliweka bayana kile wanachofanya.