Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuna wasiwasi na cambodia baada ya chama cha upinzani kufutwa: Zeid

Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’aad al-Hussein. UN/Jean-Marc Ferré

Tuna wasiwasi na cambodia baada ya chama cha upinzani kufutwa: Zeid

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein ameonyesha hali  ya wasiwasi  juu ya kuwepo kwa uwazi na uhuru kwenye uchaguzi nchini Cambodia baada ya mahakama kuu nchini  humo  kufuta usajili wa chama kikuu cha upinzani kwa miaka mitano.

Chama hicho, CNRP ambacho ni kikuu cha upinzani Cambodia kimekuwa kinapinga uamuzi wa mahakama kuzuia uhuru wa vyombo vya habari nchi humo huku wizara ya mambo ya ndani ikidai kuaw kimekuwa kikipanga  njama za mapinduzi dhidi ya serikali.

Bwana Zeid  amesema demokrasia yenye ufanisi inahitaji upinzani ambao unaweza kufanya kazi kwa  uhuru bila vitisho , ameongeza kuwa  matukio hayo yote ni  kiashirio cha ukiukwaji wa haki za binadamu, na pia ukiukwazi wa haki za kukusanyiko  kwa mujibu wa sheria ya kimataifa.

Ikumbukwe kuwa rais wa  chama hicho cha CNRP  Kem Sokha alifungwa mnamo tarehe 3 Septemba wa mwaka 2013 kwa mashtaka ya uasi .