Uhalifu dhidi ya wahamiaji Libya unaweza kuwajibishwa kupitia ICC
Uhalifu dhidi ya wahamiaji waliofungwa au kusafirishwa kwa njia haramu kupitia Libya unaweza kuwajibishwa chini ya mamlaka ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC.
Kauli hiyo imetolewa na mwendesha mashtaka wa ICC, Bi Fatou Bensouda, akihutubia kikao cha Baraza la Usalama kilichokutana leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kujadili hali nchini Libya.
Bi Bensouda amesema iwapo ukatili mkubwa unaendelea kutekelezwa , kwa kutumia mkataba wa Roma hata sita kutoa tangazo la kukamatwa kwa wahalifu wanaotekeleza vitendo hiyvo.
Aidha ametoa wito kwa mamlaka za kijeshi kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia sheria za kimataifa na sheria za kibinadamu.
Kwa mantiki hiyo amesema ofisi yake itaendelea kutathmini ukatili unaotekelezwa dhidi ya wahamiaji wanaopitia Libya.
(Sauti ya Bensouda)
“Kulingana na taarifa kamili na mazingira yatakayojitokeza katika uchunguzi wetu, ukatili kama huo huenda ukawa kesi katika mahakama hii. Suala hili ni lazima litatuliwe kesi kwa kesi, kutokana na taarifa sahihi na tathmini chini ya ofisi yangu.”