Brazil inatakiwa kuendeleza vita dhidi ya utumwa wa kisasa UM

8 Novemba 2017

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa  leo wametoa wito kwa serikali ya Brazil kuchukua hatua za haraka katika  mapambano  dhidi ya utumwa wa kisasa unaodhoofisha kanuni za ushirika.

Urmila Bhoola ambaye ni mtalaam huru wa haki za binadam wa Umoja wa Mataifa amesema, vitendo vya utumwa wa kisasa vinaongeza nchini humo na ni hali inayotia wasiwasi kufuatia maamuzi ya wizara kifungu namba 1129 kinachopunguza  kutilkia mkazo mapampano dhidi ya vitendo vya utumwa wa kisasa.

Amesema  Brazili mara nyingi imekuwa mstari wa mbele  katika kupambana na utumwa wa kisasa, hivyo maamuzi hayo ni ya kushangaza na kukatisha tamaa kuona nchi hiyo ikipoteza  dira katika swala la kupambana na vitendo hivyo.

Halidhalika Surya Deva, ambaye  ni mwenyekiti wa jopo la wataalam wa haki za binadamu wa  Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kibinadamu , pia ameonyesha wasiwasi kwamba hali hii itairudisha Brazil nyuma katika vita vyake dhidi ya utumwa wa kisasa.

Wataalam wa haki za binadamu wamepongeza juhudi za  Mahakama Kuu ya nchi hiyo kwa kutoa amri ya kusimamishwa kwa muda  maamuzi hayo ya wizara, na kuhimiza Serikali kuizuia kabisa maamuzi hayo.