Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna mwamko wa masomo ya STEM kwa vijana-Olwendo

Kuna mwamko wa masomo ya STEM kwa vijana-Olwendo

Masuala ya kisayansi na hususan masomo ya sayansi yamewapa vijana motisha na hivi sasa kundi hilo linaonekana kuwa na mtazamo chanya kuhusu masomo hayo kwani wametambua fursa zinazoweza kupatikana kikazi kufuatia kujikita na masomo hayo.

Hii ni kauli ya Dkt Joseph Ouko Olwendo, mhadhiri katika chuo kikuu cha Pwani nchini Kenya anayehudhuria mkutano wa masuala ya anga uliondaliwa kwa ushirikiano wa Umoja wa Mataifa na falme za nchi za kiarabu UAE unaondelea Dubai.

image
Dkt Joseph Ouko Olwendo, mhadhiri katika chuo kikuu cha Pwani nchini Kenya . (Picha:UNVideoCapture)
Mkutano huo umeleta pamoja wadau mbali mbali kutathmini matumizi ya teknolojia ya anga katika maendeleo endelevu.

Ameongeza kuwa ili kuchagiza wanawake na wasichana kuingia kwenye masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati,  au STEM.

(Sauti ya Olwendo)

Aidha Dkt. Olwendo ametaja umuhimu wa kushiriki katika mkutano huo akisema..

(Sauti ya Olwendo)