Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bodi ya wakurugenzi wa UM yakutana Nairobi Kenya

Bodi ya wakurugenzi wa UM yakutana Nairobi Kenya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliyewasili Nairobi Kenya leo ataongoza mkutano wa bodi ya wakurugenzi CEB utakaoanza kesho mjini Nairobi.

Mkutano huo unawaleta pamoja wakuu wa mashirika yote ya Umoja wa Mataifa, vyombo vya fedha na mipango ya mfumo wa Umoja wa Mataifa. CEB ni chombo kinachotumika kuratibu majukumu ya mashirika ya Umoja wa Mataifa katika nchi mbalimbali kuhusu masuala ya kijamii, kiuchumi na mengineyo.

Na pia kinasaidia kuimarisha mfumo wa Umoja wa Mataifa ili kuhakikisha unatekeleza majukumu yake ipasavyo katika masuala mbalimbali yaliyotolewa na jumuiya ya kimataifa. Ramadhan Kibuga anaarifu.

(SAUTI YA RAMADHAN KIBUGA)