Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jukwaa laanza Bahrain likiangazia ujasiriamali na SDGs

Jukwaa laanza Bahrain likiangazia ujasiriamali na SDGs

Jukwaa la kimataifa kuhusu uwekezaji katika ujasiriamali linaanza leo huko Manama nchini Bahrain kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya uwekezaji, ujasiriamali na malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Shirika la maendeleo ya viwanda la Umoja wa Mataifa, UNIDO limesema jukwaa hilo linafanyika Bahrain kwa kuzingatia jinsi nchi hiyo iko mstari wa mbele kusongesha ujasiriamali kama njia ya kufanikisha amani, ustawi na uwezeshaji wa kiuchumi duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Manama, mkuu wa UNIDO kitengo cha uwekezaji, teknolojia na uhamasishaji nchini Bahrain Dkt. Hashim Hussein amesema ni kwa kuzingatia hoja hiyo, Bahrain inatumia mkutano huo wa siku tatu kuonyesha harakati zake na zaidi ya yote..

(Sauti ya Dkt. Hussein)

“Jambo muhimu kwenye jukwaa hili ni maudhui yake. Kufanikisha SDGs kupitia ujasiriamali na uwekezaji, na unafahamu kikao cha 72 cha Baraza Kuu kinalenga watu na kufanikisha amani. Kwa hiyo tunapozungumzia watu na vichocheo vya uchumi kwetu sisi tunawaitawajasiriamali. Kwa hiyo inafanyka kwa wakati muafaka na Bahrain inachukua nafasi yake duniani kuzungumzia ustawi, amani, haki na uwezeshaji uchumi wa watu.”