Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yaanisha vipaumbele kwa mwaka 2011

UN yaanisha vipaumbele kwa mwaka 2011

Kitengo cha Umoja wa Mataifa ambacho kimeanzishwa kwa ajili ya kushughulia masuala ya wanawake UN Women, kimetangaza mpango wake mkakati wa wa siku 100 ambao utafuatilia na kutoa ushirikiano kwa nchi mbalimbali dunia ili hatimaye kusukuma mbele ustawi wa wanawake.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kitengo hicho Michelle Bachelet mpango huo umetuwama kwenye maeneo matano ambayo ni pamoja na kutilia uzito utelezaji wa maazimio ya kimataifa kwa nchi wanachama, kuunga mkono mikakati inayoshukuliwa na jumuiya za kikanda kwa ajili ya kuleta usawa wa kijinsia pamoja na kuongeza sauti katika uso wa dunia ili kuleta mapinduzi ya utoaji elimu na taarifa kuhusiana na usawa wa kijinsia.

Kitengo hicho cha Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya wanawake kilianzishwa July mwaka jana kufuatia azimio lilipitishwa na baraza la usalama baada ya kuunganishwa vitengo mbalimbali ndani ya Umoja huo vilivyokuwa vikishughulikia masuala ya wanawake. Kitengo hicho ambacho kimetengewa fedha za kutosha kinatazamiwa kuzinduliwa rasmi mwezi ujao wa February.