Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ikibidi nguvu itumike kulinda wananchi:Ban London

Ikibidi nguvu itumike kulinda wananchi:Ban London

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa umoja huo unapaswa kutekeleza majukumu yake ipasavyo ili kuwalinda wananchi dhidi ya majanga yasababishwayo na binadamu pamoja na yale yatokanayo hali ya asili, lakini hata hivyo amesisitiza kuwa jumuiya za kimataifa zinaweza kuingilia kati na kutumia nguvu pale inapoonekana mamalaka za kidola zinashindwa kuliwanda wananchi wake.

Akizungumza kwenye mhadhara wa chuo kikuu cha Oxoford Ban amerejelea kubainisha misingi ya uundwaji wa Umoja wa Mataifa akisema kuwa umoja huo unatambua haki na wajibu uliopo kwa mamlaka za dola ambazo zinapaswa kuwalinda na kuwatetea wananchi wake dhidi ya matukio kama vita, uonevu na mahijaji mengine ya kibinadamu, lakini inapofika pahala hayo yanapuuzwa,jumuiya za kimataifa zinawajibika kuingilia kati.

Ametolea mfano maazimio yaliyipitishwa kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2005 ambao viongozi wa dunia waliafiki kuchukua jukumu la kulinda na kupinga vitendo vyovyote vya mauwaji ya halaiki, maangamizi ya kutisha, mapigano ya kikabila pamoja na dhulma yoyote dhidi ya utu wa mwanadamu.

Amesema viongozi wa dunia wanawajibika kuhakikisha kwamba wanatilia uzito hayo yote yaliyokubaliwa kwa ajili ya mustaabala mwema wa binadamu.