Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume za UM ni nguzo ya kuleta maendeleo:Migiro

Tume za UM ni nguzo ya kuleta maendeleo:Migiro

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro amesisitiza kuwa tume za kimaeneo za Umoja wa Mataifa ndiyo nguzo katika juhudi za Umoja wa Mataifa za kupunguza umaskini na kunua maisha ya watu.

Akiongea kwenye mkutano wa mashirika ya kuchumi ya bara la Amerika kusini na Caribbean mjini Santiago Chile, bi Migiro amesema kuwa malengo ya kiuchumi , kijamii na kimazingira ni lazima yashirikishwe kwenye mipango yote pamoja na sera.

Bi Migiro amesema kuwa tetemeko la ardhi nchini Haiti na Chile sawia na mafuriko yaliyotokea nchini Brazil vimeonyesha sababu ya kuwepo kwa miundo mbinu na nyumba ambavyo vinaweza kustahimili gali mbaya ya hewa na pia kuwepo kwa maendeleo mengine ya muda mrefu.

Bi migiro ameongeza kuwa ni lazima kuwe na ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa , serikali na wafanyibiashara ili kubuni njia za kutekeleza maendeleo ya kudumu.