Neno la wiki: Shimizi

20 Oktoba 2017

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia neno "Shimizi".  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Nuhu anasema Shimizi ni vazi ya siri ambayo wanawake wanalivalia ndani ya nguo ama wanavaa wakati wanalala. Amesema ni aina fulani ya rinda inachovaliwa kwenye sehemu ya mabega hadi magotini....na anailinganisha na vesti inayovaliwa na wanaume..