Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tofouti za Supu na Mwengo ni zipi?

Neno la wiki - Supu na Mwengo

Tofouti za Supu na Mwengo ni zipi?

Wiki hii tunaangazia maneneno “Supu" na "Mwengo” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema sio kila kitu ambacho kimepikwa katika maji ni Supu. Mwengo ni aina ya supu itokanayo na kupika viumbe vya bahari kwa maji, kama vile samaki, pweza, ngisi. Ukitaka kuagiza supu yake unasema naomba mwengo wa samaki, mwengo wa pweza au mwengo ya ngisi...