Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya walimu duniani, walimu wanena

Siku ya walimu duniani, walimu wanena

Ikiwa leo ni siku ya walimu duniani, yenye kuli mbiu ya kufundisha kwa uhuru huwezesha walimu. wanataaluma hao wameeleza maoni yao siku hii ikiadhimishwa ambapo pia wamezungumzia wajibu wa jamii katika kutimiza lengo lao. Selina Jerobon na taarifa kamili.

(Taarifa ya Selina)

Mashirika ya Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO, la kazi duniani ILO, la kuhudumia watoto UNICEF na la mpango wa maendeleo UNDP katika taarifa yao ya pamoja kuadhimisha siku hii yamesema mara nyingi waalimu hawana uhuru na msaada wanaohitaji ili kutimiza majukumu yao.

Yamesisitiza kwamba walimu ndio msingi muhimu kwa kila jamii wakitaka nchi zote duniani kutambua mchango wao, kuwawezesha na kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili.

image
Mwalimu akiwa darasani akifundisha. (Picha:UNESCO)
Katika mahojiano na Tumaini Anatory wa redio washirika Karagwe Fm, Kagera nchini Tanzania, walimu wameeleza jinsi ambavyo uhuru wa kufundisha unawezesha maendeleo ya taaluma.

(Sauti Walimu)

Siku ya walimu duniani inayoratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, inaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 20 ya mapendekezo ya shirika hilo kuhusu hadhi ya walimu wa elimu ya juu ikilenga zaidi uhuru wa taasisi na taaluma sanjari na kauli mbiu ya mwaka huu.