Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili ukisuasua, mamilioni ya wakimbizi Mashariki ya Kati mashakani

Ufadhili ukisuasua, mamilioni ya wakimbizi Mashariki ya Kati mashakani

Msimu wa baridi kali ukikaribia, mustakhbali wa wakimbizi na wakimbizi wa ndani huko Mashariki ya Kati uko mashakani kutokana na kupungua kwa ufadhili.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linasema hali hiyo inatia wasiwasi kwa kuzingatia kuwa ni robo tu ya wakimbizi walioko kwenye ukanda huo ndio wanaweza kupata usaidizi wa kujiandaa na msimu huo wa baridi kali.

Kwa mujibu wa UNHCR wakimbizi wapatao milioni 15 kutoka Syria na Iraq wamesambaa kwenye nchi mbalimbali za Mashariki ya Kati ikiwemo Jordan na Misri likisema milioni 4 kati yao watakumbwa na janga kubwa.

Hadi sasa ombi la dola milioni 245 kwa ajili ya usaidizi wakati wa msimu wa baridi kali kwa mwaka 2017/2018 limefadhiliwa kwa asilimia 26 tu.