Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchakato wa kutokomeza nyuklia uwe shirikishi- Lajčák

Mchakato wa kutokomeza nyuklia uwe shirikishi- Lajčák

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao cha ngazi ya juu kuhusu kutokomeza silaha za nyuklia wakati huu ambapo kuna tishio kubwa la matumizi ya silaha hizo. Selina Jerobon na ripoti kamili.

(Taarifa ya Selina)

Nats..

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres akianza hotuba yake kwenye kikao hicho akibainisha kuwa matukio ya hivi karibuni ya majaribio ya silaha za nyuklia, yamefanya kikao cha leo kiwe muhimu zaidi.

Ametumia kikao hiki kilicholeta pamoja wawakilishi wa nchi wanachama na mashirika yasiyo ya kiserikali kueleza kile kinachotokea sasa..

image
jaribio la kombora kutoka DPRK. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili
(Sauti ya Guterres)

“Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea imefanya msururu wa majaribio ya kichochezi ya makombora ya nyuklia na kuibua hofu na hatari za kuenea silaha.”

Kama hiyo haitoshi, amesema kuna mgawanyiko mkubwa baina ya nchi kuhusu kutokomeza silaha za nyuklia, akisema kuwa anatambua changamoto zilizopo.

Hata hivyo amesema silaha za nyuklia madhara yake hayatambui mipaka na ndio maana..

(Sauti ya Guterres)

“Dunia isiyo na silaha za nyuklia ni dira ya dunia nzima inayotaka hatua za kimataifa.”

Mapema akifungua mkutano huo, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Miroslav Lajčák  amesema..

“Tunapaswa kuhakikisha kuwa mjadala huu unashughulikia mitazamo tofauti ya nchi wanachama. Mafanikio yetu yanategemea ni kwa jinsi gani mchakato huu ulivyo shirikishi.”