Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ADD International yachukua hatua kufanikisha SDGs

ADD International yachukua hatua kufanikisha SDGs

Malengo ya maendeleo endelevu SDGs yamewekewa ukomo wa kutekelezwa ambao ni mwaka 2030. Kwa mantiki hiyo Umoja wa Mataifa unataka kila mtu ashiriki ipasavyo ili asiachwe nyuma. Kwa kusema kila mtu, ina maana bila kujali rangi, jinsia au muonekano wake. Ni kwa mantiki hiyo shirika lisilo la kiserikali la ADD International ambalo linachukua hatua za kusaidia watu wenye ulemavu kwa maendeleo, limejikita katika nchi tano Afrika na Asia ili kusaidia watu wenye ulemavu. Je shirika hilo linafanya nini? Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Jimmy Innes, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo ambalo ameshiriki baadhi ya vikao kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani wakati wa mjadala wa wazi wa Baraza Kuu. Hapa anaanza kwa kuelezea kile ambacho wanafanya.