Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajali za barabarani zimefurutu ada lazima zikome:UM

Ajali za barabarani zimefurutu ada lazima zikome:UM

Kila mwaka watu zaidi ya milioni 1.2 wanauawa katika ajali za barabarni , lakini juhudi zinafanyika ili kupunguza kiwango hicho kwa kiasi kikubwa amesema afisa wa Umoja wa Mataifa.

Jean Todt mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kuhusu usalama barabarani ameyasema hayo wakati wa kongamano la kimataifa kuhusu kanuni za Magari ambalo limesisitiza kwa nchi kutekeleza miongozo inayojumuisha mahitaji ya usalama na miundombinu bora ya barabara.

Bwana Todt amesema maendeleo yaliyo sanjari na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG’s yanaweza kuleta mabadiliko makubwa katika nchi zinazoendelea ambako zaidi ya vifo 9 kati ya 10 vya ajali za barabarani vinatokea.

(JEAN TODT)

“Kwa bahati mbaya bado tunakabiliwa na changamoto ya asilimia 90 ya wahanga wanatoka katika nchi zinazoendelea, hawajui kutumia miakanda ya usalama, hawataki kuvaa kofia za kujikinga, hawana miundombinu bora ya barabara, wana magari kuukuu. Hivyo tunahitaji kushughulikia tatizo hilo sasa nan chi hizo.”