Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takriban robo tatu ya watoto na vijana wanakabiliwa na ukatili na usafirishaji haramu :IOM, UNICEF

Takriban robo tatu ya watoto na vijana wanakabiliwa na ukatili na usafirishaji haramu :IOM, UNICEF

Takriban robo tatu ya watoto na vijana wanakabiliwa na ukatili, unyanyasaji na usafirishaji haramu wa binadamu katika safari za wahamiaji kupitia bahari ya Mediterranea, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa, la uhamiaji IOM na la kuhudumia watoto UNICEF . Flora Nducha na taarifa kamili...

(TAARIFA YA FLORA)

Ripoti hiyo “safari za machungu” inasema wahamiaji na wakimbizi watoto na vijana wanaojaribu kuingia Ulaya wanakabiliwa na kiwango kikubwa cha ukiukwaji wa haki za binadamu na asilimia 77 ya wanaosafiri kupitia Mediterranea ya Kati wakiripoti unyanyasaji na vitendo vingine vya usafirishaji haramu.

Kwa mujibu wa msemaji wa IOM Leonard Doyle ripoti inaonyesha wakati wahamiaji na wakimbizi wakiwa katika hatari , vijana na watoto wako katika hatari zaidi kuliko watu wazima wa umri wa miaka 25 na zaidi

(SAUTI YALEONARD DOYLE)

“wahamiaji na wakimbizi 22,000, wakiwemo watoto na vijana 11,000 waliohojiwa na IOM., imejikita zaidi katika hali inayowakabiliwa wahamiaji wanaopitia Libya , mara nyingi wanafanyiwa ukatili na unyanyasaji na wasafirishaji haramu wakiwa mahabusu. Nadhani ripoti hii inadhihirisha hatari inayowakabili watoto na manyanyaso yao.”