Operesheni za kunasua miili baada ya maporomoko Sierra Leone yaendelea

Operesheni za kunasua miili baada ya maporomoko Sierra Leone yaendelea

Nchini Sierra Leone wakati harakati za usaidizi kwa wahanga wa maporomomo ya udongo yaliyotokea zaidi ya wiki mbili zilizopita zikiendelea, juhudi nazo zinaendelea kuopoa miili ya watu waliopoteza maisha.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linasema baadhi ya sehemu za miili ya binadamu zinapatikana kwenye mto Juba karibu na mji mkuu Freetown kama anavyoelezea Jesse Kinyanjui, afisa wa masuala wa huduma za kujisafi wa UNICEF nchini humo.

(Sauti ya Jesse)

Yaelezwa kuwa zaidi ya miili 500 imepatikana huku mamia kadhaa bado hawajulikani walipo na watu zaidi ya 6,000 wamepoteza makazi yao ambapo kwa mujibu wa Bwana Kinyanjui, serikali ya Sierra Leone imeamua kuwa watu wote waliopoteza makazi yao wawepo kwenye kambi mbili ili kurahisisha huduma za misaada akisema..

(sauti ya Jesse)