Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Japan yatoa dola milioni 10 kusaidia wakimbizi, Uganda

Japan yatoa dola milioni 10 kusaidia wakimbizi, Uganda

Serikali ya Japan imetoa mchango wa dola milioni kumi kama uitikio wao kwa mahitaji yanangezeka katika jamii ya wakimbizi na wenyeji Kaskazini mwa Uganda kutokana na mmiminoko wa wakimbizi kutoka Sudan Kusini. John Kibego na maelezo Zaidi.

(Sauti ya Kibego)

Mwakilishi wa Shirka la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) nchini Uganda,, Bornwell Kantande amewapongeza Wajapani kwa uitikio wao kwa janga la wakimbizi nchini Uganda, na kuongeza kuwa mchango huo utasaidia kushughulikia matakwa ya baadhi ya wakimbizi waliohatarini zaidi pamoja na wenyeji, amabo wamekubali kuendeela kupokea na kuishiriki rasilimali zao na wakimbizi wa Sudan Kusini.

Kwa mchango huo wa dola milioni 10, UNHCR inachukua milioni nne halikadhalika Shirika la kuhudumia watoto UNICEF na lile la mpango wa chakula duniani (WFP), yatachukua dola tatu kila moja.

Mchango huo umepokewa wakati idadi ya wakimbizi inaongezeka kila uchao nchini Uganda sasa ikiwa ni nyumbani kwa Zaidi ya milioni moja na laki tatu, takriban milioni moja wakiwa ni Wasudan Kusini.