Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikosi cha kikanda Sudan Kusini ni fursa kwa UNMISS kushika majukumu mengine

Kikosi cha kikanda Sudan Kusini ni fursa kwa UNMISS kushika majukumu mengine

Kuwasili kwa kikosi cha kikanda nchini Sudan kusini maana yake wanajeshi wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS ambao tayari wako juba wanaweza kupelekwa katika maeneo mengine nchini humo ili kulinda raia, kusaidia kufikishwa kwa misaada ya kibinadamu, kufuatilia na kutoa taarifa kuhusu haki za binadamu. Amina Hassan na taarifa zaidi

(TAARIFA YA AMINA )

Hayo yamesemwa na mkuu wa UNMISS David Shearer, ambaye pia ni mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini humo alipozungumza na waandishi wa habari mjini Juba, akisema kuwasili kwa kikosi kutoka Rwanda, ukiongeza na wanajeshi wa Nepal na wahandisi zaidi ya 100 wa Bangladesh katika eneo hilo ni fursa kwa askari wa UNMISS kushika majukumu mengine

(SHEARER CUT 1-KIBEGO)

“UNMISS kila wakati inatathimini vipaumbele vyake, kupata wanajeshi wa ziada kunamaanisha tunaweza kufanya majukumu mengine zaidi yanayoendana na wajibu wetu, kulinda raia na kujenga amani ya kudumu. Kwa mfano itatuwezesha kushika doria zaidi katika baranara zisizo salama ambako kumekuwa na mashambulizi dhidi ya misafara ya raia kama vile barabara za Juba hadi Nimule na Juba hadi Bor.”

Bwana Shearer pia amefafanua kuwa kikosi hicho cha kikanda sio jeshi jipya la walinda amani tofauti na la Umoja wa Mataifa

(SHEARER CUT-KIBEGO 2)

“ Wakati ni kikosi tofauti kwa maana ya wajibu na utekelezaji wake hapa, kinasalia kuwa chini ya usimamizi wa UNMISS hivyo kitakuwa kinaongozwa na brigedia jenerali , lakini kitakuwa chini ya kamanda wa jeshi ambaye atakuwa chini yangu, kwa hiyo ni sehemu ya UNMISS , sio kikosi kinachojitegemea.”