Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanariadha wakimbizi nchini Kenya wajiandaa kung’aa Olimpiki London

Wanariadha wakimbizi nchini Kenya wajiandaa kung’aa Olimpiki London

Wachezaji wakimbizi nchini Kenya wamejiunga na wachezaji wengine chini ya Jumuiya ya Kimataifa ya shirikisho la riadha ili washiriki katika mazoezi na michuano. Wakimbizi hao kutoka nchi jirani ikiwemo Sudan Kusini na Somalia, wamewekwa katika timu ya wanariadha wakimbizi waliochaguliwa na mfuko wa Tekla Loroupe nchini Kenya.

Tekla Loroupe ni mwanariadha mstaafu na anashikilia rekodi ya dunia ambaye alishiriki pia mbio za marathoni katika michuano mbalimbali ya kimataifa.  Wakimbizi hao wamepata fursa isiyo ya kawaida maana wanafanya mazoezi chini ya uangalizi wa wanariadha wa kimataifa wa Kenya, ikiwa ni pamoja na bingwa wa Olimpiki Bwana David Rudisha, ambaye alivunja rekodi ya dunia katika michuano ya mita 800.

Wakimbizi watakaofaulu watashriki katika michuano ya London mwezi huu wa Agosti. Hili ni tukio la kihistoria na la kipekee maana itakuwa ni mara ya kwanza wakimbizi kushirikishwa katika michezo ya aina hii ya kimataifa…. Kocha wao John Anzara anasema ana uhakika wanariadha hawa watafanya vizuri katika mashindano hayo.

Katika makala ifuatayo, Wanariadha hao wanaelezea jinsi watakavyotumia ujasiri wao kung'aa katika michuano hiyo.....ungana na Selina Jerobon kwa undani zaidi....