Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni lazima kuhakikisha magaidi hawamili silaha:Fedotov

Ni lazima kuhakikisha magaidi hawamili silaha:Fedotov

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili tishio la ugaidi katika kudumisha amani na usalama wa kimataifa.

Baraza hilo ambalo limepitisha kwa kauli moja azimio nambari 2370 la mwaka 2017 la kuwazuia magaidi kumiliki silaha limesema ili kuhakikisha amani na usalama wa kimataifa lazima nchi zishikamane kupambana na vitendo vyote vya kigaisi lakini kubwa zaidi ni kuhakikisha magaidi hao hawawezi kumiliki silaha.

Akizungumza kwa njia ya video kwenye kikao hicho kutoka Vienna mkurugenzi mtendaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa na uhalifu UNODC bwana Yury Fedotov amesema magaidi wanaweza kupata silaha kwa njia mbalimbali ikiwemo biashara haramu kwenye mtandao, udhibiti duni mipakani, na usafirishaji haramu wa silaha na kuzuia hali hiyo ndio mtihani mkubwa..

(FEDOTOV CUT 1)

“Kuzuia silaha kutoangukia mikononi mwa magaidi hilo linaleta changamoto kubwa ambayo inahitaji mshikamano, mikakati mbalimbali na hatua za kupambana na uhalifu kisheria.”

Amesema ili kukabili changamoto hizo...

(FEDOTOV CUT 2)

“Tunahitaji kuimarisha ushirika miongoni mwa nchi mipakani na operesheni za kukabiliana nao, kuchagiza ushiriki wa wadau wote ikiwemo sekta binafsi na kuboreshha uwezo wa kukabiliana na ugaidi wa kiwango kikubwa.”