Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ingawa mashambulizi yamepungua, albino bado wanaishi kwa hofu vijijini:Ero

Ingawa mashambulizi yamepungua, albino bado wanaishi kwa hofu vijijini:Ero

Watu wenye ulemavu wa ngozi au Albino katika ameneo ya vijijini nchini Tanzania bado wanaendelea kuishi kwa hofu wakati hulka ya kutaka kuwashambulia ikienea amesema mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye ulemavu wa ngozi akihitimisha ziara yake nchini humo.

Ikponwosa Ero, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es slalaam amesema kazi kubwa bado inahitajika kushughulikia suala la ushirikina na kuelimisha umma.

(SAUTI YA ERO)

“Watu wenye ulemavu wa ngozi wanaendelea kuishi katika hali tete , wakati mzizi wa mashambulizi dhidi yao ukiendelea kuenea, na athari za zaidi ya muongo mmoja wa mashambulizi zimewalipisha gharama kubwa.”

Hata hivyo baada ya ziara ya siku 11 Bi Ero amekaribisha kupungua kwa idadi ya visa vya mashambulizi vinavyoripotiwa na kuipongeza serikali ya Tanzania kwa kazi kubwa ya kukabiliana na zahma hii ambayo ni Imani potofu kwamba viongo vya albino vina thamani kubwa katika masuala ya ushirikina.

(SAUTI YA ERO2)

“Kumekuwa na hatua chanya za kushughulikia vitendo vya kishirikina , ikiwa ni pamoja na kuwafanyia usajili waganga wa kienyeji.”

Ameongeza kuwa bado kuna mvurugano kwa jamii wa kutofautisha ushirikiana na wanganga wa kienyeji suala linalohitaji elimu zaidi na kutaja saratani ya ngozi kama tishio linguine kubwa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ambalo serikali inapaswa kujitahidi kulifanyia kazi.